Riwaya ya Mungu Hakopeshwi ni riwaya iliyoshinda na kupewa tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa mwaka 2018.
Riwaya hii inaelezea maisha ya familia moja ya Unguja iliyoingia katika mitafaruku na mikasa mingi.
Kila kitu huwa na chanzo na khatima; basi ni nini chanzo cha mitafaruku hiyo na khatima yake ilikuwaje?
Simulizi ni juu ya baba, Bw. Ahmed, mwenye hasira kali zisizo na mipaka, aliyeongoza familia yake kwa utashi wa nafsi yake, bila kujali hisia za mkewe wala wanawe. Kumbe moyoni mwake alihifadhi siri, na hiyo siri ndiyo iliyomfanya Bw. Ahmed kuwa mkali bila kiasi, ikimsukuma azuie kurejea kwa yale yaliyomfika zamani. Lakini kivuli cha historia ya maisha yake ya nyuma hakikuacha kumuandama.
Riwaya hii imeandikwa kwa lugha nzuri na fasaha, kwa ufundi wa msanii makini na mwelewa wa maisha ya jamii za Kizanzibari na za mwambao kwa ujumla.
“In Mungu Hakopeshwi, Zainab Alwi Baharoon, has used the standard unguja Swahili masterfully. The language used flows so effortlessly that the reader can also have fun while reading. The overriding issue handled in this work is women’s struggles against the backdrop of male chauvinism and domination where the women find themselves at the bottom rung of the societal ladder (especially in the Swahili society).” – The Judges (Mabati-Cornell Kiswahili Prize for Literature, 2018)
top of page
SKU: 9789987753932
Ksh1,150.00Price
Out of Stock