top of page

Nilipomaliza ilikuwa saa nane kamili. Wakati huo, Pendo alikuwa bado hajalala ila alisinziasinzia. Niliiacha ile karatasi mezani. Nikadatama kwenye kochi tayari kulala. Usingizi ulikuwa umenishika kwa mang’amung’amu kisha nikagutushwa na mtu. Nilifikiria ni makusudi lakini nilipotazama alikuwa Pendo. Alikuwa ametoka kitandani kuja kulala nilipokuwa. Nilishtuka! Niliamka na kuketi.

“Pendo? Kuna shida gani?” nilimuuliza.
“Siwezi kulala peke yangu!” alinijibu.
“Sasa uko peke yako ama tu pamoja?” nilimsaili.
“Niko pekee! Kitandani peke yangu!” alinijibu kimzaha
“Nami sijazoea kulala na mtu!” nilimpasha.

Mfanisi anaanza safari yake ya kujisaka punde akiwa shuleni katika madarasa ya malezi na chekechea. Anatembea katika dunia hii ambayo anajiona akiwa pekee katika ulimwengu wa familia za wazazi wote wawili, kinyume naye aliye na mama pekee. Dunia yake inampelekea kuwa na marafiki tofauti tofauti kuanzia Moi’s Bridge huko Kenya, Mwanza Tanzania na mara tena Nakuru na Mombasa nchini Kenya. Maisha yake, kimsingi yanaathiriwa pakubwa na ama marafiki zake au familia yake.

Katika riwaya hii utakumbana na maudhui mseto yanayoathiri kizazi cha leo na kijacho. Imeyaangazia maudhui mbalimbali kama vile maisha katika ndoa, mahusiano ya vijana kwa vijana, mahusiano ya wazee kwa vijana na wazee kwa wazee, talanta, elimu, bidii na kazi, usaliti katika maisha, unafiki, siasa na uongozi n.k. Ni kazi inayomulika maisha ya leo na jinsi masuala ibuka yanayoathiri jamii kwa namna hasi au chanya na ni kazi ya aina yake na ambayo hutajutia kuiweka mkononi kuisoma.

Safari Ya Matumaini by John Wanyonyi

SKU: 9789987081806
Ksh990.00Price
Quantity

    You May Also Want...

    bottom of page