Mamangu Nipe Wosia ni diwani inayotoa mafunzo na maonyo kwa vijana ili waweze kwenda katika njia zifaazo maishani. Maudhui yake yaliyobebwa na neno ‘mama’ yana nguvu ya uzazi na ulezi ndani yake iliyo na uwezo wa kumwongoza hata kijana yatima au yule aliyekosa mausia yaliyo mema. Fauka ya hayo, si diwani iliyojikunyata mithili ya kifaurongo, kwani ukiachana na masuala ya malezi, imeangazia pia siasa, uhifadhi wa mazingira, maisha na kifo, uanamajumui, mapenzi na masuala mengine kadha wa kadha ambayo yamejadiliwa kwa mitindo tafautitafauti iliyosukwa kwa ufundi wa hali ya juu.
Mamaangu Nipe Wosia
SKU: 9789987082209
Ksh650.00Price
















