top of page

Sauti dhaifu ya kilio cha mwanamke ilinifikia pale nilipokuwa nimesimama karibu na vichaka vikubwa vilivyoshonana mbele yangu. "Hivi ni sauti ya binadamu kweli au ni mlio wa mnyama fulani?" Nilijiuliza swali hilo ingawa sauti ile niliyoisikia ilifanana sana na kilio cha mwanamke ambaye yuko katika maumivu makali. Hali fulani ya woga ilianza kuniingia polepole. Baada ya kuanza kupatwa na woga niliamua kumfuata bibi yangu ambaye nilimwacha akiendelea kukata kuni nyuma ya vichaka vingine vilivyokuwa kushoto kwangu. Baada ya kutembea kwa hatua zisizozidi kumi nilimwona bibi akinifuata. Hapo niliamua kusimamana kumsubiri ili nim-wulize juu ya ile sauti niliyoisikia. "Nimesikia sauti kama ya mtu ambaye alilia kwa muda mrefu na mwisho akapoteza nguvu". Bibi yangu alieleza hivyo kabla ya mimi kumweleza. "Hata mimi nilisikia ile sauti, tena inaelekea ni sauti ya mwanamke. Hivi unavyoniona ndio nimeamua kutofuata tena hizo kuni, maana nimeanza kuogopa."

Kilio Cha Mwanamke by Idrissa Haji Abdalla

SKU: 9789987084975
Ksh990.00Price
Quantity

    You May Also Want...

    bottom of page