top of page

Kichuguu kinawavutia wapita njia nao wanakigeuza mtaji. Hamadi! palipokuwa na kuchuguu panazaa ufuska, vurugu na visa tele. Linakuwa jiji la raha na karaha zote? Mgodi wa Mbovili. Mgodi unaotema madini na kutunisha mifuko ya wengi waingiao na kuwapa kiburi kisichomithilika.

Mgoli naye hali bado kinda, ananaswa kwenye tandabui la huba la mwalimu wake, Mkebe, aliyetumia mwanya wa hali ngumu ya maisha ya Mgoli kumrubuni kwa kumpatia vijisenti vya matumizi. Huba linampeleka puta Mgoli, hata ashindwe kujinasua. Husemwa haba na haba hujaza kibaba na kinga na kinga ndipo moto uwakapo. Mgoli aliyeonja asali, anajiingiza katika penzi jingine la Babu Jimi, mfanyabiashara maarufu wa madini. Akiwa na wanaume hawa wawili, Mgoli anapata ujauzito. Haya baba wa mtoto ni nani? Na nini hatma ya Mgoli?

Kuhusu Mwandishi

Athumani Mauya ni Mwalimu mstaafu kutoka Bagamoyo. Anaishi jijini Dar es Salaam na familia yake. Riwaya yake nyingine iliyochapishwa na Mkuki na Nyota ni ‘Harusi ya Dogoli’

Kibanda Cha Mkaa by Athumani Mauya

SKU: 97899877531471
Ksh490.00Price
Quantity

    You May Also Want...

    bottom of page