top of page

Tumbili anakiiba kinanda cha mzee Tumbo. Anakiiba kinanda hicho kuwatumbuiza wanyama wa pori wanaofika kwenye himaya yake kila siku ili kusakata rumba wawili wawili. Tumbili anajipata mashakani baada ya kubainika kuwa kinanda chake chenye mvuto wa sauti kilikua kifaa cha mzee Tumbo. Hukumu yake ilikua mijeledi ishirini kwa shtaka la kwanza, na mijeledi mingine ishirini kwa shataka la pili pamoja na kazi ya sulubu; Kazi ya Nyani na Tembo indhihirika punde tu hukumu inapotolewa. Je, Tumbili atastahimili adhabu hiyo? 

 

Soma hadithi ya Tumbili na Kinanda ufahamu kilichomfika Tumbili baada ya hukumu kutolewa kuhusu wizi uliotokelezea.

Tumbili na Kinanda by Stanley Gazemba

SKU: 9789966623201
Ksh450.00Price

    You May Also Want...