Nyaraka za siri zimeibiwa kutoka ofisi moja ya wapigania uhuru jijini Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania inaingiwa na hofu kuwa nyaraka hizo zitaishia mikononi mwa adui na kuhatarisha maisha ya watu wengi wasio na hatia. Kutokana na ishara maalumu inasadikiwa kuwa majasusi hao wamekimbilia jijini Nairobi. Mpelelezi nguli, Willy Gamba, anapewa kazi ya kuwatafuta popote walipo, kwa gharama yoyote na kuwapokonya nyaraka hizo. Kazi hiyo lazima ifanyike haraka kabla hawajaziuza kwa adui. Muda unazidi kwenda na mapambano ya kuwasaka majasusi hao yanazidi kuwa makali na hakuna huruma. Pande zote zinapoteza watu muhimu. Wapelelezi, majasusi na raia wengine wasio na hatia wanauawa. Wakati wote huo Willy Gamba anaendelea na upelelezi wake mgumu na ndipo anapokutana na mrembo Lina. Lakini mrembo huyu yuko upande gani? Na Lulu je? Je, Chifu yupo sahihi anapomwonya Willy Gamba asimwamini mwanamke yeyote mrembo? Willy Gamba na wenzake wanabanwa vilivyo lakini hawana ruhusa ya kushindwa. Maisha ya wengi yanawategemea. Ni mapambano ya kufa na kupona, lakini wanawashindaje maadui wakali kama hawa?
top of page
SKU: 9789987083138
Ksh450.00Price
Out of Stock