top of page

Ebrahim Hussein lililofanyika mwaka 2015/16. Tunzo hiyo ilianzishwa
na hayati Gerald Belkin, muongoza filamu aliyekuja Tanzania
kutengeneza filamu juu ya maisha na changamoto za ujenzi wa
ujamaa vijijini miaka ya 1960 na 1970. Belkin alifanya kazi bega
kwa bega na Profesa Ebrahim Hussein, mwanazuoni maarufu na
mwandishi wa tamthilia na mashairi. Kupitia kwa Hussein, Belkin
alivutiwa na utamaduni wa Kiswahili, hususani ushairi. Katika wosia
wake, kabla ya kufikwa na mauti, aliacha fungu la fedha ili zitumiwe
kushindanisha washairi wa Tanzania, na tunzo itolewe kwa washindi
watatu wa kwanza. Belkin alianzisha tunzo hii ili kuuenzi mchango
wa rafiki yake, Ebrahim Hussein, katika kuijenga fasihi ya Kiswahili.

Ebrahim Hussein ametoa mchango mkubwa katika utunzi, uchambuzi
na falsafa ya fasihi. Vitabu vyake, kwa mfano Kinjeketile, Mashetani,
Wakati Ukuta na Kwenye Ukingo wa Thim vimebeba fikra nzito juu ya
migogoro ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni inayotokana
na mabadiliko ya kihistoria nchini Tanzania na barani Afrika kabla na
baada ya uhuru. Ni jambo la kusikitisha kuwa kazi hizo bora hivi leo
hazipatikani kwa wingi wala kufundishwa shuleni nchini Tanzania.

Diwani hii ni chapisho la pili la Tunzo ya Ebrahim Hussein. Bodi ya
Tunzo iliamua kwamba tungo bora za shindano kwa kila awamu
ziwe zikichapishwa katika Diwani ili ziweze kusomwa na watu wengi
zaidi. Hivyo, Diwani hii maalumu ya pili ina mashairi teule ya washindi
na washiriki wengine wa shindano, pamoja na tafsiri za Kiingereza
za mashairi ya washindi watatu wa kwanza. Diwani nyingine zitakuwa
zikichapishwa kadiri shindano linavyoendelea kufanyika.

Mashairi haya yametungwa na washairi mchanganyiko – vijana,
watu wazima, wazee, wanawake, wanaume, wafanyakazi, wasomi,
wakulima, n.k. Kwa pamoja, mashairi haya yanatusawiria hali ya
Tanzania na Afrika katika kipindi hiki, na kubainisha mitazamo anuai
ya wananchi wa kawaida kuhusu hali hiyo na kuhusu mustakabali wa
nchi yao na bara lao la Afrika. Diwani hii inafaa kusomwa na watu
wote wanaojali hali na hatima ya Mwafrika.

DIWANI YA TUNZO YA USHAIRI YA EBRAHIM HUSSEIN JUZUU LA KWANZA by Ebrahim Hussein

SKU: 9789987753895
Ksh890.00Price

    You May Also Want...